Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Glory, MD
ULY CLINIC
5 Juni 2025, 14:27:15
Mtoto wa kiume kucheza tumboni
Swali la msingi
Hisia za mtoto wa kiume kucheza tumboni?
Majibu

Kucheza kwa mtoto wa kiume tumboni (kupiga buti au kujongea) ni jambo la kawaida kabisa na ni ishara njema kwamba mtoto anaendelea vizuri. Lakini kwa kweli, mpaka sasa tafiti zinaonyesha kuwa uwezo wa kuhisi mtoto kucheza tumboni hauhusiani na jinsia ya mtoto, yaani mtoto wa kiume au wa kike kwa kuwa wote huweza kuleta hisia zinazofanana.
Mambo ya muhimu kuhusu mtoto kucheza tumboni
Kuanza kucheza
Mama mjamzito huanza kuhisi mtoto kucheza kwa mara ya kwanza (kuitwa quickening) kati ya wiki ya 16 hadi 25 ya ujauzito. Kwa mama wa mara ya kwanza, mara nyingi ni karibu na wiki ya 20.
Harakati hutofautiana
Wengine huhisi mateke makali, wengine ni kama kusukumwa au kupuliziwa hewani. Harakati huwa nyingi zaidi wakati mama amepumzika au baada ya kula.
Kucheza sana hakumaanishi mtoto ni wa kiume
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba watoto wa kiume wanacheza sana au zaidi ya wa kike. Hali hii hutegemea mtoto binafsi, nafasi aliyolala tumboni, na hali ya afya ya ujauzito.
Harakati ni kiashiria cha afya ya mtoto
Kupungua kwa harakati za mtoto hasa baada ya wiki ya 28 ni jambo la muhimu kufuatiliwa—ikiwa mtoto anaonekana kupunguza kucheza, mama anashauriwa kuwasiliana na mtoa huduma wa afya mara moja.
Ushauri muhimu
Mama anaweza kufuatilia harakati za mtoto kwa kuhesabu “kicks” mara kwa mara (mfano: angalau mara 10 kwa saa 2 baada ya kula). Endelea na kliniki kwa ufuatiliaji wa karibu wa ukuaji wa mtoto na maendeleo ya ujauzito.
Rejea za mada hii:
RCOG. Reduced Fetal Movements. Royal College of Obstetricians and Gynaecologists Green-top Guideline No. 57. London: RCOG Press; 2011.
ACOG Committee Opinion No. 828. Clinical management guidelines for obstetrician–gynecologists: management of stillbirth. Obstet Gynecol. 2021;137(2):e63–e76.
Heazell AEP, Froen JF, Tveit JVH, Flenady V, Midbari A. Detection and management of decreased fetal movements in pregnancy: a survey of obstetric practice in the United Kingdom. J Obstet Gynaecol. 2008;28(6):496–9.
Rayburn WF. Fetal body movements: clinical significance and research directions. Obstet Gynecol Clin North Am. 1999;26(4):707–21.
O’Sullivan O, Stephen G, Martindale E, Heazell AEP. Predicting poor perinatal outcome in women who present with decreased fetal movements: a prospective cohort study. PLoS One. 2013;8(7):e69784.
Winje BA, Wojcieszek AM, Gonzalez-Angulo LY, Piaggio G, Heazell AEP, Flenady V. Interventions to enhance maternal awareness of decreased fetal movement: a systematic review. BJOG. 2016;123(6):886–98.
Sadovsky E, Yaffe H. Daily fetal movement recording and fetal prognosis. Obstet Gynecol. 1973;41(6):845–50.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
