top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

15 Juni 2025, 08:31:47

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Mzunguko wa hedhi

Mzunguko wa hedhi ni mchakato ambao mfumo wa uzazi wa mwanamke hupitia kila mwezi ili kutotoa yai kutoka kwenye ovari na kuweka uwezekano wa kupata mimba sambamba na kubomoa kwa ukuta uliotengenezwa endapo ujauzito hautatokea. Vitendo hivi hutokea kwa kujirudia na kwa wanawake wengi hutokea kwa katika muda wa siku 21 hadi 45.


Kuingia mwezini ni kitendo cha kuvuja damu kila mwezi kutoka kwenye uke ambapo hutokea mwanzoni mwa kila mzunguko wa hedhi. Kuvuja huku husababishwa na kubomoka kwa ukuta wa ndani ya kizazi uliotengenezwa kwa ajili ya upokea yai lililochavushwa.


Mambo yanayotokea katika mzunguko wa hedhi

  • Yai hukomaa na kutototolewa (mchakato unaoitwa utotoleshaji au uovuleshaji)

  • Ukuta wa ndani ya kizazi  huvimba pamoja na kuongezeka kwa mishipa ya damu hivyo kuwa tayari kupokea yai lililorutubishwa na shahawa za mwanaume

  • Yai lililotungishwa hujipachika kwenye ukuta wa ndani ya kizazi na kuanza kukua NA

  • Yai lisipotungishwa, halijipachiki, na ukuta ndani ya kizazi huanguka na kutolewa kama damu ya hedhi.


Kukokotoa siku za mzunguko wa hedhi

Siku za mzunguko wa hedhi huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya mzunguko mmoja wa hedhi. Kwa kawaida mzunguko mmoja wa hedhi huweza kuchukua siku kati ya siku 21 na 45 hata hivyo huweza kubadilika kati ya mwezi mmoja na mwingine. Kwa kawaida, kipindi cha hedhi hudumu kwa siku 3 hadi 7.

  • Wasichana huanza kupata mzunguko wa hedhi wakati wa kubalehe, wakiwa na na umri wa miaka 13, na hukoma kupata hedhi katika wakati wa komahedhi, wakiwa na umri wa miaka 52

  • Ovari hutaga (kutaga yai) takribani siku kati ya siku 7 hadi 31 kabla ya kuanza kwa mzunguko wa hedhi mwingine ikitegemea urefu wa mzunguko wako wa hedhi

  • Mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kupata mimba ikiwa atafanya mapenzi bila kinga wakati wa siku 3 hadi 5 kabla ya kutaga yai au siku ya kutaga yai. Hivyo kufanya kuwa na siku za hatari 6 katika mzunguko mmoja w ahedhi.


Je, ni matatizo gani yanayoweza kutokea kwa mzunguko wa hedhi?

Kwa kawaida matatizo makubwa ya mzunguko wa hedhi ni pamoja na:

  • Kuvuja damu nyingi au kwa wakati usio sahihi

  • Maumivu ya hedhi

  • PMS (ugonjwa wa kabla ya hedhi)

  • Komahedhi kabla ya wakati


Sababu za kutoingia hedhi

Sababu za kawaida zaidi za kutoingia mwezini katika mzunguko wa hedhi ni:

  • Ujauzito

  • Komahedhi


Rejea za mada hii
  1. Marc Manual. Menstruation. https://www.msdmanuals.com/sw/home/women-s-health-issues/biology-of-the-female-reproductive-system/menstrual-cycle. Imechukuliwa 12.11.2024

  2. Mihm M, et al. The normal menstrual cycle in women. Anim Reprod Sci. 2011 Apr;124(3-4):229-36. doi: 10.1016/j.anireprosci.2010.08.030. Epub 2010 Sep 3. PMID: 20869180.

  3. Adams Hillard PJ. Menstruation in adolescents: what's normal? Medscape J Med. 2008;10(12):295. Epub 2008 Dec 30. PMID: 19242601; PMCID: PMC2644006.

  4. Grieger JA, et al. Menstrual Cycle Length and Patterns in a Global Cohort of Women Using a Mobile Phone App: Retrospective Cohort Study. J Med Internet Res. 2020 Jun 24;22(6):e17109. doi: 10.2196/17109. PMID: 32442161; PMCID: PMC7381001.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page