top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

8 Juni 2025, 06:58:30

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Penadur injection inatibu nini?

ree

Penadur ni jina la kibiashara la dawa Benzathine Penicillin G, ambayo ni antibiotiki iliyogunduliwa miaka mingi iliyopita na na imekuwa ikitumika kwenye matibabu ya maambukizi ya bakteria.


Dawa hii hutumiwa kwa kuchoma sindano kwenye misuli katika matibabu ya magonjwa yanayosababishwa na bakteria wanaodhuriwa na dawa, sambamba na kutumika kama kinga ya homa ya baridi yabisi na maambukizi ya streptococcus kooni.


Magonjwa yanayotibika na Penadur injection

Kama maelezo ya awali, penadur injection hutibu maambukizi ya Streptococcus ambayo hutokea kwenye ko, ngozi na sehemu nyingine ya mwili mathalani;

  • Hutumika kama kinga ya homa ya baridi yabisi na ugonjwa wa moyo wa baridi yabisi

  • Hutibu kaswende na maambukizi mengine anayosababisha kimelea Treponema

  • Hutibu magonjwa ya ngozi kama Yaws, Bejel, na Pinta

  • Hutumika kama kinga dhidi ya bakteria kwenye figo kama kutokana na bakteria Streptococcus


Maudhi ya penadur injection

Baadhi ya maudhi ya kawaida ya penadur injection yanayotokea sana huwa kama yafuatayo;

  • Maumivu au uvimbe kwenye sehemu ilipochomwa sindano

  • Homa au kuhisi baridi

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Upele wa ngozi mdogo


Madhara ya penadur injection

Baadhi ya maudhi makubwa au madhara ya penadur injection ni pamoja na;

  • Mzio Mkali unaoambatana na dalili za kupumua kwa shida, kuvimba uso, midomo, au koo

  • Sindromu ya Stevens-Johnson ambapo ni mwitikio mkali unaosababisha ngozi kupata malengelenge makubwa.

  • Mwitikio wa kinga wa Jarisch-Herxheimer wakati wa matibabu ya Kaswende – Dalili za mafua kutokana na bakteria kufa ghafla

  • Madhara ya mfumo wa neva ikiwa imeingizwa kimakosa kwenye mshipa wa damu (degedege, kuchanganyikiwa)


Watu wasiopasa kutumia penadur injection

Watu wafuatao wanapaswa kutotumia penadur injection kuepuka madhara isipokuwa endapo wameshauriwa na daktari;

  • Wanaosumbuliwa na mzio na dawa jamii ya Penicillin au Cephalosporins

  • Wenye pumu kali au historia ya mzio mkali

  • Wajawazito (matumizi tu kwa ushauri wa daktari)

  • Wenye ugonjwa wa figo (huenda wakahitaji marekebisho ya dozi)


Rejea za mada hii
  1. Walker GJ,et al. Antibiotic treatment for newborns with congenital syphilis. Cochrane Database Syst Rev. 2019 Feb 15;2(2):CD012071.

  2. Ndeikoundam Ngangro N, et al, referents for the regional offices of the French national public health agency. Pillonel J, Lot F. Bacterial sexually transmitted infections in France: recent trends and patients' characteristics in 2016. Euro Surveill. 2019 Jan;24(5)

  3. Webber BJ, et al. Chemoprophylaxis against group A streptococcus during military training. Prev Med. 2019 Jan;118:142-149.

  4. Struyve M, et al. Primary syphilitic proctitis : case report and literature review. Acta Gastroenterol Belg. 2018 Jul-Sep;81(3):430-432.

  5. Khan A, et al. An old disease re-emerging: acute rheumatic fever. Clin Med (Lond). 2018 Oct;18(5):400-402.

  6. Gozdas HT, Dogan A. Is Benzathine Penicillin the Treatment of Choice in Neurosyphilis? Am J Med. 2023 Oct;136(10):e208.

  7. Dündaröz R, et al. Evaluation of DNA damage using the comet assay in children on long-term benzathine penicillin for secondary prophylaxis of rheumatic fever. Pediatr Int. 2001 Jun;43(3):276-80.

  8. Kingston M, Carlin E. Treatment of sexually transmitted infections with single-dose therapy: a double-edged sword. Drugs. 2002;62(6):871-8.

  9. Benzaken AS, et al. Adequacy of prenatal care, diagnosis and treatment of syphilis in pregnancy: a study with open data from Brazilian state capitals. Cad Saude Publica. 2019;36(1):e00057219.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page