top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

15 Juni 2025, 08:46:50

Urithi wa kundi la damu kwa mtoto

Uvumbuzi wa makundi ya damu kwa mfumo wa ABO uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliyopita ulileta furaha kwa wanasayansi Duniani kwa sababu ulisaidia kukabiliana na tatizo kubwa la madhara yaluiyokuwa yanatokea kwa kuongezewa damu isiyo sahihi kwa fikra kwamba damu za watu zinafanana.


Uvumbuzi huo ulianzisha safari nyingine ya kuelewa kuwa kundi la damu hurithiwa kizazi hadi kizazi na kundi la damu la mtoto anayezaliwa hutegemea makundi ya damu ya wazazi wake.

Makala hii imeeleza kuhusu urithishaji wa makundi ya damu kwa watoto kwa kuzingatia makundi ya damu ya wazazi.

 

Aina ya makundi ya damu


Kuna makundi makuu 4 ya damu ambayo ni A, B, AB, na O. Watu wenye kundi O la damu hawana antijeni A wala B licha ya kuwa na afya njema.


Mwaka 1910 iligundulika kuwa makundi haya yad amu hurithiwa, na kundi A na B antijeni hutawala katika urithi.


Urithishaji wa makundi ya damu ni kama yalivyoelezewa kwenye jedwali na 1 hapa chini


Jedwali na 1: Ulithishaji wa kundi la damu kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto

Maelezo ya ziada ya jedwali namba 1

  • Endapo baba ni kundi A, na mama ni Kundi A, mtoto atakayezaliwa huwa na damu kundi A

  • Endapo baba ni kundi A na mama ni kundi B, Mtoto atakayezaliwa huwa kundi AB

  • Endapo baba ni kundi A na mama ni kundi O, mtoto atayezaliwa huwa ni kundi A

  • Endapo baba ni kundi B, na mama ni Kundi A, mtoto atakayezaliwa huwa na damu kundi AB

  • Endapo baba ni kundi B na mama ni kundi B, Mtoto atakayezaliwa huwa kundi B

  • Endapo baba ni kundi B na mama ni kundi O, mtoto atayezaliwa huwa ni kundi B

  • Endapo baba ni kundi O, na mama ni Kundi A, mtoto atakayezaliwa huwa na damu kundi A

  • Endapo baba ni kundi O na mama ni kundi B, Mtoto atakayezaliwa huwa kundi B

  • Endapo baba ni kundi O na mama ni kundi O, mtoto atayezaliwa huwa ni kundi O


Rejea za mada hii
  1. Reid ME et al. The Blood Group Antigen Facts Book. Second ed. 2004, New York: Elsevier Academic Press.

  2. Daniels G. Human Blood Groups, Second ed. 2002, Blackwell Science.

  3. Stayboldt C , Rearden A , Lane TA . B antigen acquired by normal A1 red cells exposed to a patient's serum. Transfusion. 1987;27:41–4.

  4. Reid ME , et al. Associations between human red cell blood group antigens and disease. Transfus Med Rev. 1990;4:47–55.

  5. O'Donnell J , et al. The relationship between ABO histo-blood group, factor VIII and von Willebrand factor. Transfus Med. 2001;11(4):343–51.

  6. Fuchs CS , et al . Gastric carcinoma. N Engl J Med. 1995;333:32–41.

  7. Sazama K . Reports of 355 transfusion-associated deaths: 1976 through 1985. Transfusion. 1990;30:583–90.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page