Shiriki Utafiti wa Afya leo na upete ZAWADI ya muamala wa Fedha💸
Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
Imeandikwa:
29 Aprili 2026, 13:59:15

Tunakuomba ushiriki katika tafiti muhimu inayolenga kuboresha huduma za afya nchini Tanzania kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa ya Akili Unde (AI) kwa lugha ya Kiswahili.
Mada ya Utafiti
Uundaji, Utekelezaji, na Tathmini ya Athari ya Jukwaa la Afya ya Kidijitali linalotumia Akili Unde (AI) kwa Kiswahili ili kuongeza uelewa wa Afya miongoni mwa Wagonjwa na Wahudumu wa Afya wa ngazi ya kati nchini Tanzania
Lengo la Utafiti
Utafiti huu unalenga kuchunguza namna ambavyo jukwaa la afya ya kidijitali linalotumia AI kwa Kiswahili linaweza kusaidia wagonjwa pamoja na wahudumu wa afya kupata elimu sahihi ya afya, kuongeza uelewa wa magonjwa mbalimbali, na kuboresha mawasiliano ya afya kwa urahisi zaidi.
Kupitia tafiti hii, tunatarajia kusaidia jamii kupata taarifa za afya kwa lugha rahisi na inayoeleweka vizuri zaidi.
Kwa Nini Ushiriki Wako ni Muhimu?
Maoni yako yatasaidia:
kuboresha huduma za afya kidijitali nchini Tanzania
kuongeza upatikanaji wa elimu ya afya kwa Kiswahili
kusaidia maendeleo ya matumizi ya AI katika sekta ya afya
kujenga mfumo bora wa kusaidia wagonjwa na wahudumu wa afya
Kila mchango wako una thamani kubwa katika maendeleo ya afya ya jamii.
Faida ya Kushiriki
Baada ya kukamilisha kujaza fomu ya utafiti, utapata zawadi ya muamala kidogo kama shukrani kwa muda wako na ushiriki wako.
Pia unaweza:
Kushiriki na rafiki yako ili naye ashiriki na kupata zawadi yake pia.
Kadri watu wengi wanavyoshiriki, ndivyo mchango wa kuboresha afya ya jamii unavyokuwa mkubwa zaidi.
Usiri wa Taarifa
Taarifa zako zote zitahifadhiwa kwa usiri mkubwa na zitatumika kwa madhumuni ya utafiti pekee. Hakuna taarifa binafsi zitakazotolewa kwa mtu mwingine bila ruhusa yako.
Idhini ya Utafiti
Namba ya Idhini ya IRB: KUIRB-2026-0025-01
Utafiti huu umeidhinishwa rasmi kufanyika kwa kufuata maadili ya utafiti wa kisayansi.
Karibu Ushiriki Sasa
Jaza fomu ya utafiti, pata msimbo wako wa uthibitisho, tuma msimbo huo kwa namba iliyotolewa, na upokee zawadi yako.
Asante kwa kuwa sehemu ya mabadiliko ya afya nchini Tanzania.
Namna ya Kushiriki
Fungua linki iliyoambatana na picha hii, kisha nenda kwenye boksi la meseji na uliza swali lolote la afya. Utapokea majibu, na chini yake utaona linki ya “Shiriki”.
Bofya linki hiyo, jaza fomu ya utafiti na utume. Baada ya hapo utaelekezwa kwenye ukurasa wenye msimbo wako wa uthibitisho. Tuma msimbo huo kwa maelekezo utakayopewa ili upokee muamala wako wa fedha haraka.
Imeboreshwa
1 Mei 2026, 09:51:25
