Uboreshaji wa ujuzi- Tabibu
Nyumbani
Mgonjwa
Daktari
Elimu Afya
Pata tiba
Ujauzito
Mlo Afya
Mafunzo
Dawa A-Z
Blogi
Dalili & Viashiria A-Z
Magonjwa A-Z
Virutubisho A-Z
Mengineyo
Fomu hii inachukua maelezo muhimu kutoka kwako yatakayomsaidia daktari kutambua tatizo ulilonalo na kukupa matibabu yanayoendana nawe. Tafadhali jaza taarifa za ukweli kwa kadri unavyofahamu. Tunazingatia sera yetu ya usiri na faragha kuchakata taarifa zako na ni siri baina yako na daktari wako.
Sehemu A: Demografia
Anza na Kodi ya nchi mfano kwa Tanzania ni +255
Sehemu B: Historia ya Mgonjwa
Ugonjwa wowote sugu ni kama UKIMWI, Kisukari, Shinikizo la juu la damu, Pumu n.k
Magonjwa ya ngozi ni kama Vidonda vya Herpes Midomoni au Ukeni au umeni, Chunusi, Mkanda wa Jeshi Saratani ya ngozi, Melanoma, Kupoteza nywele mwilini, Muwasho kichwani, Ngozi kavu, Soriasis, Rosacea, Pumu ya ngozi n.k.
Andika magonjwa mengine ya ngozi kama yapo ambayo hayajaorodheshwa kwenye swali na 9
Jaza kama umejibu una ujauzito kwenye swali 14 hapo juu
Orodhesha dawa zozote unazotumia kwa sasa ambazo si za kutibu tatizo ulilonalo sasa.
Mfano
Parasetamo Vidonge vitatu mara tatu kwa siku.
Dawa za kuyeyusha damu nikama Aspirin, Coumadin Plavix na mafuta ya samaki
Sehemu C: Historia ya tatizo la ngozi Lililopo sasa
Taja sehemu ya mwili ambako tatizo lilianza kwa mara ya kwanza.
Taja sehemu zote zilizoathirika. Ikiwezekana eleza upande wa mwili, kwa mfano mkono wa kulia, mguu wa kushoto, uso, kifua, mgongo au sehemu za siri.
Eleza unachoona kwenye ngozi, kwa mfano vipele, mabaka, vidonda, malengelenge, ngozi kukauka, ngozi kuchubuka, kuvimba, kubadilika kwa rangi, kutokwa na usaha, damu au majimaji.
Eleza kama tatizo huongezeka kutokana na joto, jasho, kuoga, sabuni, vipodozi, chakula, dawa, kugusa sehemu hiyo, kujikuna, mwanga wa jua, msongo wa mawazo, nguo fulani au jambo lingine.
Eleza kama kuna dawa, krimu, kuosha, kuweka kitu kwenye ngozi, kukaa sehemu yenye baridi, kuepuka kitu fulani au jambo lingine linalopunguza dalili.
Kwa mfano kutumia sabuni mpya, mafuta au krimu mpya, vipodozi, dawa, kemikali, manukato, bidhaa za nywele, nguo mpya, chakula kipya, kufanya kazi na kemikali, kuumwa au kung'atwa na mdudu, au kugusana na mtu mwenye tatizo la ngozi.
Andika taarifa yoyote ambayo haijaulizwa hapo juu lakini unadhani inaweza kumsaidia daktari kuelewa tatizo lako.
Kwa mfano kutambua chanzo cha tatizo, kupata ushauri wa matibabu, kujua kama unahitaji vipimo au kujua kama tatizo ni la dharura.
Bofya kiboksi kuweka tiki kukubaliana kuwa maelezo uliyotoa hapo juu ni ya kweli kwa jinsi unavyofahamu.