Kurasa hii imeorodhesha homon mbalimbali zinazopatikana kwenye mwili wa binadamu
GLUCAGON LIKE PEPTIDE 1 (GLP-1)
Homoni ya glukagoni inayofayofanana na peptaidi (Glucagon like peptide 1) ni homoni inayozalishwa kwenye mfumo wa gastrointestino kufuatia mwitikio wa chakula kinacho ingia tumboni, hujulikana kwa jina jingine la incretin.
Erythropoietin (Erithropoietini) ni homoni inayozalishwa na figo kwa asilimia 90 na kwa kiasi kidogo sana huzalishwa na Ini, homoni hii huwa na kazi kuu ya kuchochea urojo wa mifupa(bone marrow) kuzalisha chembechembe nyekundu za damu.
Kalsitonini (Calcitonin) ni homoni inayozalishwa na seli C za tezi ya thairoidi, Homoni hii huwa na kazi kuu ya kuthibiti kiasi cha madini ya Calcium na phosphate kwenye damu na kusimamisha utendaji wa homoni ya parathairoidi