Mwandishi;
Mhariri:
Imeboreshwa
Dkt. Benjamin L, MD
Dkt. Salome A, MD
2 Aprili 2026, 12:09:07

Kinga ya kiungulia
Kiungulia ni maumivu yanayohisiwa sehemu ya katikati ya kifua, nyuma na chini ya miishio ya fupa titi na mara nyingi hutokana na kucheua tindikali iliyo tumboni.
Kiungulia inaweza kuwa dalili ya ugonjwa ambao hauendani na ugonjwa ulionao sasa. Mfano wa hali na magonjwa yanayoweza kusababisha kiungulia ni:
Kula vyakula vyenye viungo kwa wingi
Kunywa pombe
Kuvaa nguo za kubana
Namna ya kujikinga jna kiungulia
Ili kuzuia kiungulia, unapaswa kufanya mambo yafuatayo;
Kuepuka kuulaza mwili wako kwa angalau masaa 2 mara baada ya kula
Epuka kutumia vyakula vilivyosheheni mafuta, na uchachu
Epuka kula chocolate
Kutumia dawa za kuzuia uzalishaji tindikali tumboni
Wakati gani wa kuonana na daktari haraka?
Tafuta msaada wa haraka endapo unapatwa na dalili zifuatazo:
Maumivu ya kifua yanayoambatana na kutokwa jasho au kuishiwa pumzi au maumivu yanayoelekea kwenye mkono, taya au bega la kushoto
Dalili hazisikii dawa za kuzuia uzalishaji tindikali
Unaweza weka miadi ya kuonana na daktari endapo una dalili zifuatazo:
Unapatwa na kiungulia mara nyingi kwa wiki
Unashindwa kulala kwa sababu ya dalili za kiungulia
Unapata kikohozi kipya
Kiungulia hakiponi licha ya kutumia dawa
Unapoteza uzito bila sababu
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeandikwa;
2 Aprili 2026, 12:09:07
