Mwandishi;
Mhariri:
Imeboreshwa
Dkt. Benjamin M, MD
Dkt. Mangwella S, MD
2 Aprili 2026, 12:09:07

Kuishi maisha bora na ualbino
Tatizo la u albino huambatana na madhaifu kwenye ngozi na macho. Mtu mwenye u albino anaweza kupata tiba mazingira kwa ajiri ya kupunguza au kuepuka madhara yanayoweza kutokea. kama yaliyoorodheshwa hapa chini.
Kujikinga na mwanga wa jua
Wagonjwa wenye tatizo la ualbino wa macho, macho yao yanahitaji kukingwana mwanga mkali wa jua katika maisha yao yote. Wazazi na wa athirika wa tatizo hili wanahitaji kufundishwa namna ya kujikinga au kukabiliana na mwanga wa jua kwa njia zifuatazo
Kuvaa miwani
Kupenda Kukaa kivulini kuepuka mionzi ya mwanga wa jua
Kuvaa nguo za kujikinga na mionzi ya jua, kama vile kofia na nguo za mikono mirefu, nguo maalumu
zenye uwezo wa kupunguza mionzi ya mwanga wa jua, shati yenye kola
Angalau kuwa na masaa mawili kila baada ya muda Fulani kukaa mbali na mwanga wa jua wa moja kwa
moja
Kuzuia kutumia dawa zinazoweza ongeza hisia ya ngozi kwenye mionzi ya jua
Siku gani ya kumwona daktari?
Watu wenye ualbino wanatakiwa kumwona daktari kila baada ya miezi 6 hadi 12 kufanyiwa vipimo na uchunguzi wa ngozi. Uchunguzi wa ngozi husaidia kutambua saratani ya ngozi mapema zaidi, mwathirika atatakiwa kufanya hivi kwa sababu huwa kwenye hatari ya kupata saratani ya ngozi. Uchunguzi huu ni kwa ajili ya watoto wadogo chini ya miaka 13.
Watu wazima wanatakiwa kuhudhuria clinic kila baada ya miaka mitatu hadi sita kufanyiwa uchugnuzi huu.
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeandikwa;
2 Aprili 2026, 12:09:07
