top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

13 Februari 2026, 02:53:52

Acute Hepatitis

Acute Hepatitis ni nini?

Actute Hepatitis ni ni neno la kitiba lenye jina la Kiswahili la Uvimbe mkali wa ghafla wa ini. Uvimbe mkali wa ghafla wa ini ghafla ni hali inayotokea pale ambapo ini linapata uvimbe kwenye tishu au kuharibiwa kwa muda mfupi kutokana sababu ya maambukizi, matumizi ya dawa fulani, sumu, au sababu nyingine za zinazotokea ghafla.


Dalili za Uvimbe mkali wa ghafla wa ini zinaweza kujumuisha:

  • Uchovu uliokithiri

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Maumivu upande wa juu kulia wa tumbo

  • Kukosa hamu ya kula

  • Macho na ngozi kuwa ya njano (manjano)

  • Mkojo kuwa mweusi na kinyesi kuwa chepesi

Imeandikwa:

23 Machi 2025, 08:45:16

bottom of page