top of page

Aflatoksin

Mwandishi:

ULYCLINIC

19 Julai 2021 14:17:16

Aflatoksin

Aflatoksin ni nini?


Aflatoksin ni sumu inayozalishwa sana na fangasi wenye jina la Aspergillus flavus, Aspergillus parasiticus na Aspergillus nomius.


Sumu ya aflatoxin hufanyika wapi?


Fangasi hawa hupatikana kwenye mazao mengi kama vile


 • Shayiri

 • Mahindi

 • Karanga

 • Njugu

 • Mbegu za pamba

 • Almond

 • Korosho

 • Nazi

 • Pine

 • Pekani na mazao ya mimea mingine mtama

 • Ufuta

 • Mchele

 • Viungo mbalimbali

 • Kokoa na ngano


Sumu hii ina madhara gani?


Sumu ya aflatoksin ni kihatarishi kikubwa cha saratani ya ini kwa binadamu.


Matamshi


Matamshi ya neno Aflatoksin ni 'Afla- TOk-Sin'

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 15:09:35

bottom of page