top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Februari 2026, 04:23:05

Amytropic lateral sclerosis

Amytropic lateral sclerosis

Ni neno tiba lenye jina jingine la kiswahili la Msinyao wa misuli ya pembezoni


Amyotrophic Lateral Sclerosis (ALS) ni ugonjwa sugu wa mfumo wa fahamu (neva) unaoharibu seli za mishipa ya fahamu katika ubongo na uti wa mgongo inayoratibu mjongeo wa hiari wa misuli.


Maana kwa ufupi

ALS husababisha misuli kudhoofika, kupungua ujazo(kukonda), na hatimaye kushindwa kufanya kazi, kwa sababu ujumbe kutoka ubongo kwenda kwenye misuli hukatika taratibu.


Dalili kuu

  • Udhaifu wa misuli (mikono, miguu, uso)

  • Kulemewa kuzungumza, kumeza, au kupumua

  • Kukakamaa au kutetemeka kwa misuli

  • Kupungua kwa misuli (kukonda)


Muhimu kujua

  • Akili na kumbukumbu mara nyingi hubaki salama

  • Hakuna tiba ya kuponya kabisa kwa sasa, lakini kuna matibabu ya kupunguza kasi ya ugonjwa na kuboresha ubora wa maisha

  • ALS pia huitwa Ugonjwa wa Lou Gehrig

Imeandikwa:

23 Machi 2025, 14:19:27

bottom of page