top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Februari 2026, 06:53:15

Anafailaksis

Anafailaksis

Anafailaksis (kwa Kiingereza anaphylaxis) ni mzio mkali na wa haraka unaoweza kutokea dakika chache baada ya mtu kutumia dawa, kula chakula, au kugusana na kitu kinachosababisha mzio kwake. Ni hali hatari ambayo huhitaji huduma ya haraka ya kitabibu kwa sababu inaweza kuathiri kupumua na mzunguko wa damu.


Dalili za anafailaksis

Dalili zake hujitokeza ghafla na zinaweza kuchanganyika, zikiwemo:


Dalili za jumla

  • Kupoteza fahamu

  • Kujisikia joto kali ghafla


Dalili za ngozi

  • Kuvimba kwa ngozi

  • Kutokwa jasho jingi au kupauka

  • Ngozi kupasuka au kuonekana malengelenge makubwa


Dalili za njia ya hewa

  • Kuhisi unakabwa au kubanwa shingoni

  • Kuvimba kwa ulimi na midomo

  • Kutokwa na kamasi

  • Kupiga chafya au kupumua kwa shida


Dalili za tumbo

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuharisha

  • Maumivu ya tumbo


Dalili za mzunguko wa damu

  • Mapigo ya moyo kwenda haraka

  • Mapigo ya mishipa kuwa ya kasi

Imeandikwa:

21 Julai 2021, 19:12:31

bottom of page