top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Februari 2026, 04:47:43

Analgesia

Analgesia

Ni neno tiba lenye jina jingine la Anajizia


Anajizia (analgesia) ni hali ya kupoteza au kupungua kwa uwezo wa kuhisi maumivu katika sehemu fulani ya mwili. Hutokea pale mishipa inayobeba taarifa za maumivu inapokuwa imeathiriwa, kupondwa, au kufinywa, kubanwa katika mfumo wa neva wa kati (ubongo na uti wa mgongo) au mfumo wa neva wa pembeni. Wagonjwa wenye anajizia wanaweza pia kupoteza hisia za joto, kwa kuwa njia za neva zinazosafirisha maumivu ndizo zinazohusika pia na kusafirisha hisia za kuhisi joto. Inaweza kuambatana na dalili nyingine kama parastesia (hisia za kuwashwa au kuchomachoma), kupotea kwa hisia za mtetemo, au kushindwa kutambua nafasi ya kiungo (propriosepusheni), kulingana na aina ya tatizo la neva.

Imeandikwa:

23 Machi 2025, 08:45:16

bottom of page