top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Februari 2026, 04:51:01
Anisocoria
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Anisokoria" au "Mboni zisizo sawa"
Anikosoria ni tofauti ya ukubwa wa mboni za macho kati ya 0.5 hadi 2 mm. Anisocoria hutokea kwa kawaida kwa takriban 2% ya watu, ambapo tofauti ya ukubwa wa mboni hubaki vilevile kwa muda na haibadiliki licha ya mabadiliko ya mwanga.
Hata hivyo, ikiwa anisokoria inatokana na upanukaji au unyweo wa kudumu wa mboni moja au mwitikio wa polepole au usio kamili wa mboni moja kwa mwanga, inaweza kuashiria ugonjwa wa neva. Kutambua kama mboni isiyo ya kawaida imepanuka au imekunjuka husaidia katika uchunguzi wa tatizo.
Imeandikwa:
26 Machi 2025, 15:28:54
bottom of page
