Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Februari 2026, 08:05:10
Anorexia nervosa
Anorexia nervosa ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Ugonjwa wa kisaikolojia wa kunyinyima kula" au "Anoreksia Nevosa" ambao ni tatizo la kula linalohusisha changamoto za kisaikolojia zinazoathiri jinsi mtu anavyoona chakula, mwili na afya yake kwa ujumla. Mtu anaweza kuwa na mawazo yanayosababisha kupunguza ulaji wa chakula au kupata uhusiano mgumu na chakula, na hali hii inaweza kusababisha mabadiliko ya kiafya yanayohitaji msaada wa kitaalamu
Hufahamika vema pia kwa melezo yafuatayo
"Ugonjwa wa akili wa kutohisi njaa" – Tafsiri ya kihisia inayoeleza hali ya mtu kukosa hamu ya kula kutokana na sababu za kisaikolojia.
"Tatizo la kula linalopelekea kukonda kupita Kiasi" – Maelezo ya kina yanayoeleza athari za ugonjwa huu.
"Hali ya Kujinyima Chakula kwa Hofu ya Kunenepa" – Inasisitiza sababu kuu ya anorexia nervosa, ambayo ni hofu ya unene.
Imeandikwa:
24 Machi 2025, 19:48:21
