top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

6 Februari 2026, 17:35:39

Apathy

Apathy

Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Apathi" au "kutokujali", au "kutojali"


Apathi ni hali ya kitabibu inayojitokeza kwa kupungua au kukosekana kwa hisia, hamu, au msukumo wa kushughulika na mazingira ya nje au masuala binafsi. Mtu mwenye apathi huonekana kutokuwa na motisha, kutojali shughuli za kila siku, au kukosa mwitikio wa kihisia kwa matukio yanayomzunguka. Hali hii inaweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya mfumo wa fahamu (neva), matatizo ya kisaikolojia, magonjwa sugu ya mwili (kama ya figo au mfumo wa upumuaji), pamoja na matumizi au uraibu wa pombe na dawa za kulevya.


Apathi inaweza kuhusiana na magonjwa sugu yanayosababisha mabadiliko ya tabia na sonona, na katika baadhi ya hali inaweza kuwa mojawapo ya dalili za mapema za magonjwa fulani ya neva au akili, lakini haiwezi kutumika peke yake kuthibitisha ugonjwa mkali


Imeandikwa:

26 Machi 2025, 18:34:46

bottom of page