top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Februari 2026, 03:30:39
Apraxic agraphia
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Agrafia ya apraksia" ambapo ni aina ya agrafia (kupoteza au kuharibika kwa uwezo wa kuandika) inayotokana na apraksia, yaani tatizo la mfumo wa neva linalosababisha kushindwa kupanga au kutekeleza harakati zilizozoeleka, licha ya mtu kuwa na nguvu za kawaida za misuli na uelewa mzuri wa anachotaka kufanya. Katika hali hii, mtu hushindwa kuandika kwa usahihi si kwa sababu ya tatizo la lugha, bali kwa sababu ubongo hushindwa kupanga na kuratibu mfululizo wa harakati zinazohitajika kwa tendo la kuandika.
Imeandikwa:
26 Machi 2025, 18:10:13
bottom of page
