top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Februari 2026, 04:22:51
Atopic Dermatitis
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la Dermatitisi ya Kiatopiki ni hali ya kitabibu ya muda mrefu (sugu) ya ngozi inayotokana na mchanganyiko wa sababu za kinasaba, kinga ya mwili, na mazingira. Hali hii husababisha kuvurugika kwa kuta ya ulinzi wa ngozi, jambo linalofanya ngozi iwe rahisi kukauka, kuingia vijidudu, na kutoa mwitikio mkali wa mzio. Ugonjwa huu hujitokeza kwa awamu (kuja na kuondoka), mara nyingi huanza utotoni lakini unaweza kuendelea au kuanza ukubwani.
Imeandikwa:
2 Aprili 2025, 16:01:09
bottom of page
