Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Februari 2026, 04:25:13
Atrophic vaginitis
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Atrofia ya uke" ambapo ni hali ya kitabibu inayotokea pale ambapo tishu za uke hupungua unene, unyevunyevu, na uimara wake kutokana na upungufu wa homoni ya estrojeni. Hali hii husababisha mabadiliko ya kimuundo na kifizikia katika ukuta wa uke, ikiwa ni pamoja na kukauka, kupungua kwa uwezo wa kusinyaa na kutanuka, na kuongezeka kwa uwezekano wa maumivu au michubuko.
Dalili kuu za Atrofia ya Uke
Ukavu wa uke
Kuwashwa au kuungua ndani ya uke
Maumivu wakati wa kujamiiana
Kutokwa damu kidogo baada ya kujamiiana
Kuhisi uke kuwa mwembamba au kukaza
Maambukizi ya mara kwa mara ya njia ya mkojo (kwa baadhi ya wagonjwa)
Visababishi vikuu
Kupungua kwa homoni ya estrogeni
Kukoma kwa hedhi
Kuondolewa kwa ovari (upasuaji)
Matumizi ya dawa zinazopunguza estrogeni
Kunyonyesha kwa muda mrefu
Matibabu ya saratani (kemotherapi au radiotherapi)
Imeandikwa:
29 Machi 2025, 12:57:48
