Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Februari 2026, 05:21:40
Bacterial vaginosis
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Vajinosis ya bakteria"
Vajinosisi ya bakteria (ambayo zamani ilijulikana kama Gardnerella vajinalisi na Haemophilus vajinalisi) ni hali ya kitabibu ya uke inayotokea pale ambapo uwiano wa kawaida wa bakteria waliopo ukeni umeharibika, na kusababisha kuongezeka kwa bakteria wasiokuwa walinzi (hasa Gardnerella vaginalis) na kupungua kwa bakteria walinzi aina ya Lactobacillus. Hali hii si maambukizi ya zinaa moja kwa moja, bali huongeza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa.
Ugonjwa huu husababisha kutokwa na majimaji madogo, yenye harufu mbaya ya uozo, kama samaki, wa kijani au kijivu-nyeupe, ambayo hunata kwenye kuta za uke na unaweza kufutwa kwa urahisi, huku tishu za uke zikiachwa na muonekano mzuri. Kuwashwa, wekundu, na dalili nyingine za uchokozi kwenye uke zinaweza kutokea lakini mara nyingi huwa za kiasi.
Imeandikwa:
29 Machi 2025, 15:34:45
