top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Februari 2026, 06:40:57
Ballet’s sign
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Ishara ya Ballet"
Ishara ya Ballet ni dalili ya kitabibu inayojitokeza pale ambapo misuli ya nje ya macho inayohusika na mjongeo wa macho hupooza au kudhoofika, hivyo mgonjwa hushindwa kusogeza macho juu, chini au pembeni kwa hiari licha ya mgonjwa kuwa na mjongeo wa hiari kwenye mwitikio wa mwanga katika mboni. Ishara hii ni kiashiria cha usumu wa thairoid.
Hata hivyo, kope za macho hufanya kazi kawaida, na mboni za macho huendelea kuitikia mwanga ipasavyo. Hii ndiyo sifa kuu inayotofautisha Ishara ya Ballet na aina nyingine za matatizo ya harakati za macho.
Imeandikwa:
27 Machi 2025, 11:09:54
bottom of page
