top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

16 Februari 2026, 07:26:08

Beau’s lines

Beau’s lines

Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Mistari ya Beau"


Mistari ya Beau ni mishtari myeupe ya mlalo kwenye kucha, inayoonekana kama miviringo au mbonyeo katika uso wa kucha. Mistari hii inaweza kutokea baada ya ugonjwa mkali au mwitikio wa mwili kwenye sumu.


Mstari wa Beau unaweza kuhusishwa na:

  • Ugonjwa mkali uliopita (mfano homa kali au maambukizi makubwa)

  • Upungufu wa lishe

  • Sumu mwilini au dawa kali

  • Majeraha ya kitako cha kucha

  • Mshtuko mkubwa wa mwili (msongo wa kimwili)

  • Matatizo ya mtiririko wa damu (ikiwemo kuziba kwa mishipa ya moyo)

Kina cha mstari huweza kusaidia kukadiria muda tangu tukio lilipotokea kwa sababu kucha hukua polepole.

Imeandikwa:

27 Machi 2025, 09:02:08

bottom of page