top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

16 Februari 2026, 08:25:22

Benign tumor

Benign tumor

Ni neno tiba lenye jina jingine la "Uvimbe usio saratani" au "Uvimbe usio kansa"


Uvimbe usio saratani ni ukuaji usio wa kawaida wa seli unaounda uvimbe lakini hauonyeshi tabia za uvimbe was aratani. Seli zake hukua polepole, hubaki katika eneo lake la asili, na hazisambai kwenda sehemu nyingine za mwili (hakuna metastasisi).

Kwa kawaida huwa na mipaka iliyo wazi na mara nyingi husukuma na kubana tishu jirani badala ya kuzivamia. Ingawa si hatari kama saratani, unaweza kusababisha matatizo kulingana na ukubwa na mahali ulipo.


Uvimbe huu:

  • Hukaa eneo moja

  • Hukua polepole

  • Hausambai mwilini

  • Mara nyingi hausababishi madhara makubwa isipokuwa ukibonyeza kiungo muhimu

Tofautisha na uvimbe saratani ambao huvamia na kusambaa.


Dalili zinazoweza kuonekana

  • Kinyama au uvimbe unaokua polepole

  • Mara nyingi hauna maumivu

  • Dalili hutegemea eneo ulipo (mfano kubana mishipa au viungo)

Imeandikwa:

23 Machi 2025, 11:45:16

bottom of page