top of page
Fistula
Mwandishi:
ULY CLINIC
18 Julai 2021 19:03:11

Fistula ni nini?
Fistula ni njia isiyo ya kawaida inayounganisha uso wa epithelia mbili. Njia hii huwa imefunikwa na tishu za granyulesheni pamoja na kukaliwa na bakteria.
Mfano wa fistula ni, fistula kati ya uke na kibofu cha mkojo, fistula kati ya uke na njia ya haja kubwa.
Matamshi ya neno fistula ni 'Fis- CHu-la'
Asili ya neno fistula
Neno fistula ni neno lenye asili ya Kilatini lenye maana ya kitu kinachofanana na bomba au filimbi.
Imeboreshwa,
6 Juni 2022 15:10:04
bottom of page