top of page

Gangrini tepe

Mwandishi:

15 Mei 2023 14:12:24

Gangrini tepe

Gangrini tepe ni aina ya gangrini iliyosababishwa na maambukizi ya bakteria kwenye tishu. Sehemu iliyopata maambukizi huanza kuwa na maumivu makali yanayoambatana na kuvimba, malengelenge na baadaye ngozi kubadilika rangi kuwa nyeusi, kupata mng'ao, kutoa usaha na harufu, kupotea kwa hisia au kuhisi baridi kwenye kiungo kilichoathirika.


Gangrini tepe inaweza kusababishwa na majeraha ya kuungua moto au barafu au majeraha kwenye tishu. Huweza kutokea kwa watu wenye kisukari ambao wamepata majeraha kwenye vidole vya miguu bila wao kufahamu.


Kuna aina mbalimbali za gangrini tepe ikiwa pamoja na


  • Gangrini fonia ambayo huathiri maeneo ya siri na husababishwa na bakteria Clostridium perfringens

  • Gangrini gesi ambao huathiri misuli

  • Ganrini Meleney's ambayo hutokea wiki chache baada ya kufanyiwa upasuaji

  • Gangrini ya ndani ambayo huathiri ogani ndnai ya mwili kama vile matumbo n.k


Gangrini tepe huhitaji matibabu ya haraka la sivyo hupelekea kupoteza sehemu kubwa ya viungo.

Imeboreshwa,

15 Mei 2023 16:08:14

bottom of page