top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
14 Februari 2026, 11:32:56

Inflammation
Inflammation ni neno lenye jina la kiswahili la "Uchochezi wa kinga" au "Inflamesheni"
Uchochezi wa kinga ni mwitikio wa asili wa mfumo wa kinga ya mwili unaotokea baada ya jeraha, maambukizi au uharibifu wa tishu. Katika mchakato huu mishipa midogo ya damu hupanuka na kuruhusu damu, maji ya mwili, na seli za kinga kufika eneo lililoathirika.
Matokeo yake huonekana kama:
joto la eneo (sio homa ya mwili mzima)
uvimbe
wekundu
maumivu
kupungua kwa kazi ya sehemu kwa muda
Uchochezi wa kinga ni hatua ya ulinzi na huanzisha mchakato wa uponaji wa tishu.
Imeandikwa:
23 Machi 2025, 11:45:17
bottom of page
