top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

13 Februari 2026, 07:03:09

Ishara ya ortolani

Ishara ya ortolani

Ishara ya Ortolani hufahamika pia kwa lugha nyingine ya Ortolani Sign ni kipimo cha uchunguzi wa mtoto mchanga kinachotumika kubaini nyonga iliyotenguka tayari lakini inaweza kurekebishwa katika tatizo la kuzaliwa la nyonga inayoteguka. Katika ishara hii, daktari hujaribu kurudisha kichwa cha fupapaja ndani ya kikombe cha nyonga (asetabulamu). Iwapo wakati wa kujongesha fupapaja uelekeo wa mbali na muhimili wa mwili unasikika au kuhisiwa  “mteguko wa kuingia”, basi kichwa cha fupapaja kilikuwa nje na sasa kimerudi ndani.


Hivyo, Ishara ya Ortolani huonesha nyonga iliyoteguka tayari lakini inayorekebishika

Imeandikwa:

13 Februari 2026, 06:51:12

bottom of page