top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

9 Agosti 2026, 14:55:03

Kipimo cha kuotesha majimaji ya maungio

Kipimo cha kuotesha majimaji ya maungio

Kipimo cha kuotesha majimaji ya maungio (joint fluid culture), pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kwenye majimaji ya maungio, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua bakteria au vimelea wengine wanaoweza kusababisha maambukizi kwenye maungio.


Sampuli ya majimaji ya maungio ya mwili huchukuliwa kwa kutumia sindano kupitia utaratibu unaoitwa athrosentesisi, kisha hupelekwa maabara kwa ajili ya kuotesha na kutambua vimelea. Ikiwa bakteria wanapatikana, kipimo cha usikivu wa bakteria kwenye dawa kinaweza kufanywa ili kusaidia kuchagua antibayotiki inayofaa.


Kipimo hiki ni muhimu hasa pale ambapo kuna mashaka ya maambukizi ya maungio (athraitisi ya sepsisi), ambayo yanaweza kusababisha maumivu makali, uvimbe, joto kwenye kiungo na kushindwa kutumia au kusogeza kiungo vizuri.


Sampuli ya majimaji ya maungio inaweza pia kufanyiwa vipimo vingine kama hesabu ya chembechembe za damu, uchunguzi wa fuwele na uchunguzi wa moja kwa moja, kulingana na hali inayoshukiwa.


Kumbuka: Maambukizi ya maungio ni hali inayohitaji tathmini ya haraka ya kitabibu kwa sababu kuchelewa kutibiwa kunaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa kiungo.

Imeandikwa:

8 Agosti 2026, 17:09:52

bottom of page