top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

8 Agosti 2026, 16:45:26

Kipimo cha kuotesha usaha

Kipimo cha kuotesha usaha

Kipimo cha kuotesha usaha (pus culture), pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kwenye usaha, ni kipimo cha maabara kinachotumika kubaini bakteria au vimelea wengine wanaosababisha maambukizi kwenye kidonda, jipu au sehemu yenye usaha.


Sampuli ya usaha huchukuliwa kutoka kwenye eneo lililoathirika na kupelekwa maabara kwa ajili ya kuotesha na kutambua kimelea kinachosababisha maambukizi. Ikiwa bakteria wanapatikana, kipimo cha usikivu wa bakteria kwenye dawa kinaweza kufanywa ili kubaini antibayotiki ambazo bakteria hao ni sikivu nazo.


Kipimo hiki husaidia zaidi katika majipu, vidonda vilivyoambukizwa, maambukizi ya ngozi yanayorudia au maambukizi ambayo hayajibu vizuri kwa antibayotiki. Sampuli nzuri inapaswa kuchukuliwa kutoka kwenye usaha au tishu iliyoathirika, badala ya kuchukua sampuli juu ya ngozi pekee, kwa sababu bakteria wa kawaida wa kwenye ngozi wanaweza kuchanganya matokeo.


Kumbuka: Matokeo ya kipimo yanapaswa kutafsiriwa pamoja na dalili, uchunguzi wa kidonda na hali ya mgonjwa. Kuwapo kwa bakteria kwenye sampuli pekee hakumaanishi kila wakati kwamba ndiye anayesababisha ugonjwa.

Imeandikwa:

8 Agosti 2026, 16:45:26

bottom of page