top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

21 Julai 2026, 05:57:37

Kufeli kwa kiungo

Kufeli kwa kiungo

Kufeli kwa kiungo au kwa Kiingereza Organ failure ni hali ambapo kiungo cha mwili kinashindwa kabisa au karibu kabisa kutekeleza kazi zake muhimu, kiasi kwamba mwili hauwezi kuendelea kufanya kazi kawaida bila matibabu ya haraka au msaada wa vifaa maalumu. Kufeli kwa kiungo ni hatua mbaya zaidi kuliko kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi na mara nyingi huhatarisha maisha.


Kufeli kwa kiungo kunaweza kuathiri kiungo kimoja au viungo vingi kwa wakati mmoja. Kwa mfano, figo zinaweza kushindwa kuchuja taka na maji ya ziada mwilini(kufeli kwa figo), moyo kushindwa kusukuma damu ya kutosha (Kufeli kwa moyo), mapafu kushindwa kuingiza oksijeni ya kutosha kwenye damu (kufeli kwa mapafu), ini kushindwa kutekeleza kazi zake za kimetaboliki (liver failure), au ubongo kushindwa kudhibiti kazi muhimu za mwili kutokana na majeraha au magonjwa mbalimbali.


Sababu za kufeli kwa kiungo ni nyingi na zinaweza kujumuisha sepsisi, mshituko, majeraha makubwa, magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, sumu, saratani, magonjwa ya figo au ini, na maambukizi makubwa. Matibabu hutegemea kiungo kilichoathirika na chanzo cha tatizo, na yanaweza kujumuisha dawa, upasuaji, dayalisisi, mashine ya kupumulia (ventilator), vifaa vya kusaidia moyo kufanya kazi au upandikizaji wa kiungo (organ transplantation).


Kumbuka: Kufeli kwa kiungo si sawa na kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi. Katika Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi, kiungo bado kinafanya kazi lakini uwezo wake umepungua. Katika Kufeli kwa kiungo, kiungo kimeshindwa kufanya kazi kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba hakiwezi kukidhi mahitaji ya mwili bila matibabu au msaada wa vifaa maalumu.


Tazama pia: Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi, Sepsisi, Mshituko wa sepsisi, Dayalisis, Ventilator, Upandikizaji wa kiungo.

Imeandikwa:

21 Julai 2026, 05:56:00

bottom of page