Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
21 Julai 2026, 05:52:10

Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi
Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi au ikijulikana pia kama kupungua kwa uwezo wa ogani kufanya kazi ni hali ambayo kiungo cha mwili kinapungua uwezo wake wa kutekeleza kazi zake za kawaida kutokana na ugonjwa, jeraha au hali nyingine ya kiafya. Hali hii inaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na inaweza kuathiri kiungo kimoja au viungo vingi kwa wakati mmoja.
Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi kunaweza kuathiri viungo mbalimbali kama figo, moyo, mapafu, ini na ubongo. Kwa mfano, figo zinaweza kuchuja taka kwa ufanisi mdogo, mapafu kushindwa kuingiza oksijeni ya kutosha kwenye damu, moyo kusukuma damu kwa ufanisi mdogo au ubongo kusababisha kuchanganyikiwa na kupungua kwa kiwango cha fahamu.
Hali hii inaweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sepsisi, mshtuko wa ogani, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, majeraha makubwa na sumu. Matibabu hulenga kutibu chanzo cha tatizo na kusaidia kurejesha uwezo wa kiungo kufanya kazi.
Kumbuka:Â Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi (organ dysfunction)Â si sawa na kushindwa kwa kiungo. Katika kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi, kiungo bado kinafanya kazi lakini uwezo wake umepungua. Katika kufeli kwa kiungo, kiungo kimeshindwa kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na mara nyingi huhitaji matibabu ya haraka au msaada wa vifaa maalumu.
Tazama pia:Â Sepsisi, Mshituko wa sepsisi, Kushindwa kwa figo, Kushindwa kwa moyo, dayalisisi, Ventilator.
Imeandikwa:
21 Julai 2026, 05:50:49
