top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

30 Machi 2025, 14:46:10

Labyrinthitis

Labyrinthitis

Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Maambukizi ya sikio la ndani" au "Labrinthitis"


Maambukizi ya sikio la ndani husababisha kizunguzungu mzunguko kikali kinachoanza ghafla. Kizunguzungu mzunguko hiki kinaweza kutokea mara moja tu au kujirudia kwa miezi au miaka.


Dalili zinazohusiana ni pamoja na:

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kupoteza kusikia kwa hatua

  • Mjongeo wa macho usio hiari


Hali hii hutokea kutokana na kuvimba kwa labyrinthi (sehemu ya sikio la ndani inayohusika na usawa na usikivu), na inaweza kusababishwa na maambukizi ya virusi au bakteria.

Imeandikwa:

30 Machi 2025, 14:19:24

bottom of page