top of page

Magonjwa ya kuambukiza

Mwandishi:

ULY CLINIC

24 Julai 2021 13:12:32

Magonjwa ya kuambukiza

Magonjwa ya kuambukiza maana yake nini?


Magonjwa ya kuambukiza ni yale yanayosababishwa na vimelea wa aina mbalimbali na huenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu/watu wengine wenye vimelea kwa kugusa, kula au kunywa maji, kuvuta hewa, kujamiana n.k


Mfano wa magonjwa ya kuambukiza


Mfano wa magonjwa ya kuambukiza ni

  • Malaria

  • Kifua kikuu

  • UKIMWI

  • Kisonono

  • UVIKO 19 na mengineyo


Magonjwa ya kuambukiza kwa mlipuko


Magonjwa ya kuambukiza ya mlipuko yanatakiwa kutolewa taarifa haraka kwenye mamlaka inayohusika, mfano wake ni;


  • Kipindupindu

  • Homa ya dengue

  • Ebola

  • Rubella

  • Polio

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 14:48:55

bottom of page