top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Agosti 2026, 09:22:10

Maumivu kwenye nyonga

Maumivu kwenye nyonga

Maumivu kwenye nyonga ni hali ambapo mtu hupata maumivu yanayotokea ndani ya eneo la nyonga (uwazi wa pevisi), yaani sehemu yenye viungo mbalimbali vya ndani kama mfuko wa uzazi, ovari, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo na tezi dume kwa wanaume. Aina hii ya maumivu mara nyingi haihusiani moja kwa moja na mifupa ya nyonga, bali hutokana na matatizo ya viungo vilivyomo ndani ya eneo hilo.


Sababu za maumivu kwenye nyonga zinaweza kuwa matatizo ya mfumo wa uzazi kama maumivu ya hedhi (dismenorea), endometriosisi, faibroidi, maambukizi kwenye kizazi na mirija ya uzazi (PID), uvimbe wa ovari au matatizo yanayohusiana na ujauzito. Pia yanaweza kusababishwa na matatizo ya mfumo wa mkojo kama maambukizi ya kibofu au mawe kwenye njia ya mkojo, matatizo ya utumbo, au matatizo ya tezi dume kwa wanaume.


Uchunguzi hutegemea dalili na unaweza kujumuisha uchunguzi wa tumbo na mfumo wa uzazi, vipimo vya damu na mkojo, kipimo cha ujauzito inapohitajika, ultrasound ya nyonga au vipimo vingine vya picha. Matibabu hulenga kutibu chanzo cha maumivu, kama dawa za kupunguza maumivu, antibayotiki kwa maambukizi, matibabu ya homoni kwa baadhi ya matatizo ya uzazi au matibabu maalum kulingana na ugonjwa uliogunduliwa.

Imeandikwa:

3 Agosti 2026, 09:22:10

bottom of page