top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

10 Agosti 2026, 07:12:26

Mlango wa haja kubwa

Mlango wa haja kubwa

Mlango wa haja kubwa au Tundu la haja kubwa ni tundu lililopo mwisho wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, kupitia ambalo kinyesi hutoka mwilini. Kwa jina jingine hufahaika kama mkundu


Mlango wa haja kubwa una misuli maalumu inayozunguka tundu hilo, inayosaidia kudhibiti wakati wa kutoa kinyesi. Misuli hii hujulikana kama misuli ya kufungia mlango wa haja kubwa na hufanya kazi kwa kushirikiana na misuli ya eneo la nyonga.


Eneo la mlango wa haja kubwa linaweza kuathiriwa na matatizo mbalimbali kama bawasiri, mpasuko wa mlango wa haja kubwa, fistula, maambukizi, kuwashwa na uvimbe. Maumivu wakati wa kutoa kinyesi, damu kutoka kwenye mlango wa haja kubwa, usaha au uvimbe unaoendelea vinaweza kuhitaji uchunguzi wa kitabibu.


Kumbuka: Mlango wa haja kubwa ni tofauti na msamba. Msamba ni eneo lililo kati ya sehemu za siri na mlango wa haja kubwa, wakati mlango wa haja kubwa ni tundu ambalo kinyesi hutokea.

Imeandikwa:

10 Agosti 2026, 07:12:26

bottom of page