top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Aprili 2026, 07:00:22

Aota mputo
Aota mputo au aota yenye puto ni kitendo cha sehemu ya mshipa wa damu wa aota kujaa au kuvimba kama puto na kuleta mwonekano wa kama puto lililojazwa upepo.
Aota ni mshipa mkubwa wa damu unaobeba damu yenye oksijeni mwilini. Mshipa wa aota huwa na kuta pana zenye misuli ambayo huhimili shinikizo la damu inayopita ndani yake. Hata hivyo baadhi ya magonjwa ya kuambukiza, kijeni na majeraha huweza kuharibu mshipa huu na kusababisha uwe dhaifu na kuvimba kama puto na ndio maana jina hili limetokana na mwonekano wake huo.
Imeandikwa:
25 Septemba 2024, 17:26:15
bottom of page
