Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
30 Machi 2025, 15:07:56
Multiple sclerosis
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Ugonjwa wa shambulio la mayelini" au "Sklerosisi sambavu"
Ugonjwa wa ni ugonjwa wa mfumo wa neva unaoshambulia mayelin, ambayo ni kizuizi cha mafuta kinachozunguka na kulinda nyuzi za neva (akson). Mayelin ina jukumu muhimu la kusaidia uhamaji wa haraka wa taarifa za umeme kati ya ubongo, uti wa mgongo, na sehemu zingine za mwili.
Katika ugonjwa huu, mfumo wa kinga ya mwili unaanza kushambulia mayelin, na hii husababisha uvimbe na uharibifu kwa mayelin na nyuzi za neva. Matokeo yake ni kwamba taarifa za umeme kutoka kwa ubongo hazipiti vizuri kwenye maeneo yaliyoshambuliwa, na hii inaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kimwili, hisia, na kimawazo.
Ugonjwa huu wa shambulio la mayelini unaweza kusababisha vipindi vya kizunguzungu mzunguko mapema zaidi, ambavyo vinaweza kuwa vya muda mfupi au kuendelea kwa muda mrefu.
Dalili zingine za awali za ugonjwa wa shambulio la mayelini
Kizunguzungu mzunguko cha vipindi ambacho kinaweza kuwa endelevu
Kuona vitu viwili badala ya kimoja
Kuona ukungu
Kuwashwa au kufa ganzi
Dalili nyingine zinazoweza kutokea
Mjongeo macho usio hiari
Kukosa haja kubwa
Udhaifu wa misuli
Kupooza kwa viungo
Misuli kukakamaa
Ongezeko la msisimko wa refleksi
Mtetemo wa misuli wakati wa kufanya mjongo
Ataksia (kutembea kusiko imara kutokana na matatizo ya uratibu wa mjongeo)
Ugonjwa wa shambulio la mayelini ni ugonjwa unaoweza kuja kwa vipindi na kutulia kwa muda au kuendelea polepole.
Imeandikwa:
25 Machi 2025, 11:00:09
