top of page

Tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa

Mwandishi:

ULY CLINIC

21 Julai 2021 18:33:05

Tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa

Tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa humaanisha nini?


Tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa ni tarehe inayoonyesha mwezi na mwaka ambapo dawa itapoteza uwezo wake wa kitiba. Tarehe hutanguliwa na neno Exp, au Mwisho wa matumizi au Usitumie baada ya, usitumie ifikapo.


Mfano;


  • Exp: 2/2008

  • Mwisho wa matumizi: 2/2008

  • Usitumie ifikapo: 2/2008

  • Usitumie baada ya: 2/2008


Baadhi ya dawa huharibika na kuwa sumu baada ya muda wake kuisha na hivyo kutokuwa salama kwa binadamu lakini hata hivyo baadhi yake huwa na zaidi ya asilimia 90 ya kiini cha dawa licha ya kupungua uwezo.


Kwa maelezo zaidi soma katika Makala ya muda wa mwisho wa matumizi ya dawa.

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 15:05:09

bottom of page