top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Aprili 2026, 06:05:10
TDS kirefu chake ni nini?
TDS katika tiba ni kifupisho cha neno la Kilatin "ter die sumendus" linalomaanisha kutumiwa mara tatu kwa siku. Neno hili hutumika kuamuru dawa ya kunywa itumike mara tatu kwa siku.
Unaweza kutumia pia kama kifupi cha 't.d.s.
Neno jingine linalotumika sawa na TDS
Neno jingine la Kilatini linalotumika na lenye maana sawa na 'mara tatu kila siku' ni 'ter in die' na kifupi chake ni 'tid'
Baadhi ya wataalamu hutumia maneno yafuatayo pia TID na t.i.d kumaanisha 'mara tatu kwa siku'
Mara tatu kwa siku katika tiba humaanisha dawa itumike kila baada ya masaa 8
Imeandikwa:
3 Aprili 2026, 06:03:30
bottom of page
