top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
15 Februari 2026, 16:49:03

Testicular torsion
Testicular torsion ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la "Kujiviringa kwa korodani"
Kujiviringa kwa korodani ni hali ya dharura ya kitabibu inayotokea pale ambapo mishipa inayobeba damu kwenda na kutoka kwenye korodani hujiviringa hivyo kukata mtiririko wa damu kwenda na kutoka kwenye korodani. Kukosekana kwa damu husababisha upungufu wa oksijeni (isikemia) kwenye tishu za korodani, na ndani ya muda mfupi tishu huanza kufa. Hali hii huleta maumivu makali ya ghafla, uvimbe, na korodani kuwa ngumu na nyeti sana kuguswa. Bila kurekebishwa haraka kwa upasuaji, korodani inaweza kupoteza kabisa uwezo wake wa kufanya kazi au kuhitaji kuondolewa.
Imeandikwa:
15 Februari 2026, 16:48:53
bottom of page
