top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
26 Julai 2026, 10:28:32

Tishu
Tishu ni mkusanyiko wa seli zinazofanana ambazo hufanya kazi maalumu katika mwili. Tishu huunda sehemu mbalimbali za mwili kama ngozi, misuli, mishipa ya damu na viungo vya ndani.
Katika afya ya uzazi, neno tishu mara nyingi hutumiwa kumaanisha vipande vya utando au nyama laini vinavyoweza kutoka ukeni, hasa wakati wa kuharibika kwa mimba, kujifungua au baada ya baadhi ya matibabu. Tishu hizi ni tofauti na mabonge ya damu ya kawaida na zinaweza kuwa sehemu ya utando wa mfuko wa uzazi (endometriamu) au mabaki ya ujauzito.
Maneno yanayotumika kumaanisha tishu:Â Nyama, kipande cha nyama, utando, vipande vya nyama, nyama iliyotoka ukeni.
Imeandikwa:
26 Julai 2026, 10:26:58
bottom of page
