top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
12 Aprili 2025, 09:21:23

Transition Phase of labor
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Awamu ya Mpito"au"Kipindi cha Mpito katika Uchungu wa Uzazi"
Kipindi cha Mpito katika Uchungu wa Uzazi ni awamu ya mwisho ya hatua ya kwanza ya leba, na ni mojawapo ya hatua ngumu zaidi kwa mama.
Sifa za awamu ya mpito:
Mlango wa kizazi hufunguka kutoka sentimita 8 hadi 10Â (ufunguzi kamili).
Maumivu huwa makali sana na ya karibu karibu.
Mama anaweza kupata dalili kama;
Kichefuchefu au kutapika
Kutetemeka
Kuchanganyikiwa au hasira
Kuhisi presha kubwa sehemu ya chini ya tumbo au haja ya kusukuma
Hofu au kusema hawezi tena kuvumilia
Imeandikwa:
12 Aprili 2025, 09:21:23
bottom of page
