top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

10 Agosti 2026, 06:51:03

Uke

Uke

Uke ni tundu au mfereji uliojengwa kwa misuli, unaounganisha sehemu ya nje ya mfumo wa uzazi wa mwanamke na mlango wa kizazi(shingo ya kizazi. Uke huwa sehemu ya njia ya uzazi na pia ni njia ambayo damu ya hedhi hupitia kutoka kwenye kizazi kwenda nje ya mwili.


Kwa kawaida, uke huwa na mazingira yenye tindikali kidogo yanayosaidia kudhibiti ukuaji wa vijidudu vinavyoweza kusababisha maambukizi. Pia uke huzalisha majimaji ambayo husaidia kuweka unyevu na kulinda mazingira ya uke. Kiasi na muonekano wa majimaji haya vinaweza kubadilika kulingana na hatua ya mzunguko wa hedhi, ujauzito, msisimko wa kingono na mabadiliko ya homoni.


Uke unaweza kuathiriwa na matatizo mbalimbali kama maambukizi ya fangasi, maambukizi ya bakteria, magonjwa ya zinaa, ukavu wa uke, kuwashwa, maumivu wakati wa kujamiiana na maambukizi au uvimbe wa uke. Dalili kama uchafu wenye harufu kali isiyo ya kawaida, kuwashwa sana, maumivu, vidonda au kutokwa damu kusiko kwa kawaida zinahitaji uchunguzi wa kitabibu.


Kumbuka: Uke wenye afya hauhitaji kuoshwa ndani kwa kutumia sabuni, dawa au kemikali maalumu. Uke una uwezo wa kujisafisha wenyewe, na kuingiza bidhaa mbalimbali ndani ya uke kunaweza kuvuruga mazingira yake ya kawaida na kuongeza hatari ya maambukizi.

Imeandikwa:

10 Agosti 2026, 06:51:02

bottom of page