top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
12 Aprili 2025, 09:31:52
Uterine inertia
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Moyo dhaifu wa uzazi"
Moyo dhaifu wa uzazi ni hali ambapo mji wa mimba haubani kwa nguvu ya kutosha wakati wa uchungu wa uzazi ili kusababisha kufunguka kwa mlango wa uzazi au kumsukuma mtoto kutoka.
Aina za moyo dhaifu wa uzazi
Moyo dhaifu wa uzazi tangu mwanzo wa leba
Uchungu unakuwa dhaifu tangu mwanzo wa leba. Maendeleo ya mlango wa kizazi ni hafifu au hakuna kabisa
Moyo dhaifu wa uzazi unachoka baada ya muda
Uchungu ulikuwepo mwanzoni, lakini baada ya muda mji wa mimba umechoka au kupungua nguvu. Mara nyingi hutokea kwa mama aliyechoka sana au baada ya leba ndefu
Imeandikwa:
12 Aprili 2025, 09:27:02
bottom of page
