top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Machi 2025, 15:01:55
Vaginal cancer
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Saratani ya Uke"
Dalili za saratani ya uke ni pamoja na kutokwa na damu au michirizi ya damu kunaweza kuanza baada ya kutokwa na uchafu mwepesi na wa majimaji kutoka kwenye uke. Kutokwa na damu kunaweza kutokea kwa ghafla, lakini mara nyingi hutokea baada ya tendo la ndoa au kujisafisha kwa vidole (douching). Uvimbe mgumu wenye vidonda unaweza kuwepo; maumivu wakati wa tendo la ndoa, kukojoa mara kwa mara, maumivu kwenye kibofu na tumbo la chini, kutokwa na damu kwenye haja kubwa, na vidonda vya seviksi vinaweza kujitokeza baadaye.
Imeandikwa:
29 Machi 2025, 15:01:55
bottom of page
