Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Machi 2025, 15:44:00
Vaginal candidiasis
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Maambukizi ya fangasi ukeni" au "Maambukizi ya Candida albican ukeni"
Maambukizi ya Candida albicans husababisha kutokwa na majimaji mengi, meupe, kama jibini, yenye harufu ya chachu na tamu. Kuanza kwake ni ghafla, ni kawaida kabla ya hedhi au wakati wa kutumia antibiotiki. Majimaji haya yanaweza kushikamana kidogo na mashavu na kuta za uke, na mara nyingi huambatana na wekundu na uvimbe wa sehemu za nje za uke. Mapaja ya ndani yanaweza kuwa na upele mwekundu mwepesi na michubuko inayotoka majimaji. Muwasho mkali nakuungua kwenye mashavu ya uke pia kunaweza kutokea. Baadhi ya wagonjwa hupata maumivu wakati wa kukojoa kwenye tundu la mkojo.
Imeandikwa:
29 Machi 2025, 15:44:00
