Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
7 Februari 2026, 03:31:26

Vestibular neuritis
Ni neno tiba lenye jina la ksiwahili la 'Nyuraitiz ya vestibula"
Nyuraitiz ya Vestibula
Nyuraitiz ya vestibula ni hali inayosababishwa na uvimbe wa neva vestibula ambao ni mshipa wa fahamu unayohusika na uratibu wa usawa wa mjongeo wa mwili. Hii husababisha kizunguzungu mzunguko kikali ambacho kawaida huanza ghafla na kudumu kwa siku kadhaa, lakini hakuna kelele za masikio wala kupoteza kusikia.
Dalili za Nyuraitiz ya Vestibula
Kizunguzungu mzunguko kikali, kinachoweza kuwa cha kudumu kwa siku kadhaa
Kichefuchefu na kutapika
Mjongeo wa macho usio hiari
Ataksia
Sababu na Visababishi
Nyuraitiz ya vestibula inahusishwa na maambukizi ya virusi, kama vile virusi vya homa ya mapafu au herpes simplex. Katika hali nyingi, maambukizi ya virusi yanaathiri sehemu ya vestibula ya sikio la ndani, na kusababisha kupungua kwa kazi ya uratibu usawa wa mjongeo wa mwili.
Imeandikwa:
30 Machi 2025, 16:12:04
