Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
13 Julai 2026, 08:01:25

Vipele ni nini?
Vipele (hufahamika pia kama upele au kipele) ni aina ya tatizo la ngozi linalonekana kama uvimbe mdogo ulioinuka juu ya usawa wa ngozi.
Sifa kuu za vipele
Ukubwa: chini ya sentimita 1 (≤1 cm)
Umbo:Â inaweza kuwa duara au isiyo na umbo maalum
Rangi:Â vinaweza kuwa ya rangi ya ngozi, nyekundu, kahawia, au zambarau ikitegemea na rangi ya mtu
Muundo:Â mgumu, hauna usaha kwa ndani
Ni tatizo la msingi la ngozi katika matibabu ya ngozi
Havitoi majimaji (tofauti na malenge au jibu)
Huweza kutoka kama kipele kimoja au kuwa vingi
Wakati mwingine huweza kuungana na kutengeneza plagi.
Mifano ya hali zinazotoa vipele
Chunusi (vipele vya chunusi)
Mzio wa ngozi (vipele vya mzio)
Maambukizi ya virusi au bakteria
Magonjwa ya ngozi kama likeni planasi
Tofauti na madhaifu mengine ya ngozi
Baka(mabaka):Â Huwa tambarare, hauna mwinuko juu ya usawa wa ngozi
Nundu:Â Huwa kubwa na inaingia zaidi ndani ya ngozi, huzidi ukubwa wa sentimita 1
Lenge (malenge):Â huwa na maji ndani
Hitimisho
Upele ni uvimbe mdogo, mgumu, usio na maji, ulioinuka juu ya usawa wa ngozi, na ni mojawapo ya ishara muhimu katika uchunguzi wa magonjwa ya ngozi. Upele hufahamika na waswahili kwa majina mengine kama vipele, mapele, kipele, uvimbe chini ya sentimita 1 juu ya usawa wa ngozi n.k.
Imeandikwa:
7 Aprili 2026, 04:30:27
