top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

7 Februari 2026, 00:38:30

Window Period

Window period, Dirisha la matazamio

Window Period ni neno la kitiba linalofahamika kiswahili kama "Dirisha la matazamio"


Dirisha la Matazamio ni kipindi kati ya mtu kuambukizwa Virusi vya Ukimwi (VVU) na wakati ambapo vipimo vinaweza kubaini kwa uhakika uwepo wa maambukizi hayo.


Wakati wa dirisha hili:

  • Mtu tayari ameambukizwa VVU na anaweza kuambukiza wengine,

  • Lakini bado mwili wake haujatoa kingamwili za kutosha (kwa vipimo vya kingamwili), au vinasaba vya virusi (kwa vipimo vya RNA au antijeni) havijafikia viwango vinavyoweza kugunduliwa na kipimo.


Mbali na kipimo cha VVU, kuna vipimo vingine pia vyenye dilisha la matazamio ikiwa pamoja na;

  1. Hepatitis B na C

  2. UVIKO-19

  3. Kaswende

  4. Zika virus, Dengue, na Ebola

Imeandikwa:

8 Aprili 2025, 10:09:20

bottom of page